Iko wapi Faraja Yangu

Art Type: Short Story
Artist Name: Jabir Ismail

Hapo zamani, katika kijiji kidogo, aliishi binti mdogo aitwaye Zuhara. Alikuwa na umri wa miaka 10 na kuishi na baba yake pekee. Zuhara alisoma Darasa la Tano katika Shule ya Msingi Bidi Yetu. Baba yake alijitahidi sana kumlea, lakini mara nyingi alikuwa mkali na kumzuia Zuhara kuungana na watoto wenzake. Vijana wengine wa kijiji walimnyima Zuhara nafasi ya kucheza na kuwasiliana nao, kwa sababu walimwona tofauti. Waliwazuia marafiki wake na kumlazimisha kufanya kazi ngumu, kama vile kuchota maji nyumbani kwao. Wakati shule ilipokuwa ikianza, Mwalimu wake hakuweza kuelewa kwanini Zuhara alichelewa kila siku. Zuhara alikuwa na rafiki wa karibu aitwaye Swaumu, ambaye hakujua kwamba Zuhara alikuwa akiteswa na vijana wenzake. Swaumu alimuuliza baba yake ruhusa ya kumtembelea rafiki yake, na baba yake akakubali.

Siku moja, Zuhara alipokuwa akipita wakijua vijana wa kijiji, kijana mmoja alimkashifu:
“Mbona husalimii?” Kijana mwingine akasema: “Huyu analeta dharau!” Vijana wakaanza kumpiga Zuhara. Mara ghafla, Swaumu alikuja kwa sauti kubwa akisema, “Muacheni!” Vijana walishutushwa na Swaumu na wakasimama. Swaumu akamwambia Zuhara, “Twende tuwaambie wazazi wetu.” Zuhara awali alikataa.nSwaumu alimshauri, “Kwa nini hutaki? Baba yako atakuelewa.” Hatimaye, walikubaliana kwenda kwa baba ya Zuhara na kumwambia kilichotokea. Baba yake alikubali kusikiliza na kumkaribisha kwa upendo. Swaumu akamwambia, “Baba, tunakuja kuomba ushauri. Mwanao anakabiliwa na matatizo na marafiki wake.” Baba yake Zuhara alisikiliza kwa makini, na Mwalimu aliyehudhuria pia alimwambia:
“Mwanao anakabiliwa na changamoto za shule, na hatimaye anakosa fursa ya kujifunza kwa sababu ya kutengwa.” Kuanzia siku hiyo, baba yake Zuhara alibadilika. Alianza kumpa upendo na msaada, akihakikisha anakua vizuri na kupata elimu. Zuhara, akiwa na msaada wa familia na rafiki yake Swaumu, aliendelea na masomo yake kwa bidii na kufanikisha ndoto zake.

Gallery

Share the Post: