Changamoto za Familia

Art Type: Short story
Artist Name: Falhia Issa

Golewa ni mtoto mdogo ambaye huwa anafanya kazi za ujenzi akiwa na baba yake. Hata hivyo, hali ilikuwa ngumu, na alikumbana na changamoto nyingi katika maisha yake ya kila siku. Hata walipokuwa wakirudu nyumbani, baba yake alikuwa akila chakula chote na kumuacha Golewa na njaa. Mama yake, alipoona mwanawe akiwa kwenye hali ngumu na uchovu wa utumwa wa kila siku, alihuzunika sana. Alimuacha mwanawe kwa muda akaja kumpa chakula, akimwambia:
“Baba yako amefanya makosa, lakini usijali. Hii ni chakula chako.” Ilibidi mama Golewa atafute njia nyingine ya kumpatia chakula mwanae Baba Golewa aliendelea na tabia yake ya kumfanyisha kazi ngumu Golewa na kutompatia chakula, ila siku zilivyozidi kwenda alishangaa Golewa hamuombi tena chakula wala kumsumbua kwa njaa. Hali ile ilimuuma sana na alisikitika. Aliporudi nyumbani, alimuomba msamaha mama yake na kumpa chakula cha mwanawe, akijuta kwa kitendo chake.

Hata hivyo, mama Golewa alikataa kukipokea kwa mara ya kwanza na kusema kwa utulivu:
“Sina njaa mimi, naenda kulala.”Baba Golewa, akijua alikosea, aliendelea kuomba msamaha kwa kuiba chakula cha mwanawe. Hatimaye, mama Golewa alikubali na kupokea chakula hicho cha mwanawe. Mwanawe alikula kwa furaha, akiwa na shukrani kwa upendo wa mama yake. Baada ya tukio hilo, mama yake alienda kulala nyuma ya nyumba, akajificha kidogo, lakini moyo wake ulikuwa umetulia. Aliendelea na maisha yake, akiwa na matumaini kwamba familia yao ingeendelea kwa amani na mshikamano.

Gallery

Share the Post: