Haki za Msichana

Art Type: Poem
Artist Name: Hyrat Muniri

HAKI ZA MSICHANA

Hodi hodi naingia,
Uwanjani mwaniona,
Ujumbe nawaletea,
Wasichana twaangamia.

Wasichana twaozeshwa,
Tukiwa bado wadogo,
Wavulana wanasomeshwa,
Hii si haki jamani.

Mila tamaduni mbaya,
Tusiendekeze kamwe,
Msichana ana haki,
Haki ya elimu pia.

Gallery

Share the Post: