Vikwazo

Art Type: Poem
Artist Name: Khairat Hemedi

VIKWAZO

Jina langu ni Khairat,
Shule yangu ni Twiga,
Darasa langu la tano,
Ujumbe na waletea.

Wasichana tunateswa,
Nasisi twanyamaza,
Kweli haya ni maisha,
Au mazingira duni?

Wasichana tunabeba,
Mizigo mingi mikubwa,
Kunyanyaswa na kukosa elimu bora,
Na mimba za utotoni.

Walezi na jamii pia,
Nauliza hili swali,
Kwanini mnatoa wadogo kuolewa?
Kweli haya ni maisha?

Wazazi jitahidini,
Kuwasomesha watoto,
Malezi bora na elimu,
Ndiyo njia ya mafanikio.

Gallery

Share the Post: