Profile Photo

Women Fund Tanzania- WFT

  • Public Group
  • 10 months, 2 weeks ago
  • 1

    Posts

  • 1

    Members

Description

Mfuko wa Udhamini wa Wanawake Tanzania ni shirika lililosajiliwa kama shirika lisilo la kiserikali mwaka 2008 na kubadilishwa kua mfuko wa udhamini wa wanawake mwaka 2019. Kwa Tanzania ni shirika pekee na la kwanza la mfuko wa udhamini wa wanawake.

Lengo lake kubwa ni kushiriki katika kuchangia haki za wanawake kwa kutumia fursa za mfuko huo kubadilisha maisha ya wanawake Tanzania.

Carol Mango ni Mkuu wa Programu WTF. Anasema shirika hilo linaamini wanamwake na wasichana wana nafasi kubwa sana ya kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii zao. Shirika hilo linawajenga wanawake na wanaharakati kwa kuwapa sauti na kuwalinda kupitia baadhi ya programu zilizopo hapo.

Programu hizo ni pamoja na upatikanaji wa matumizi ya ruzuku, kujengewa uwezo wa kiharakati, uhamasishaji rasilimali na namna ya kuendeleza fedha na kuimarisha ukuaji wa mfuko huu.

Programu hizi zinakusudia kukuza harakati za wanawake na kupata fursa za wanawake kutoka sekta na mashirika mbalimbali kukutana na kufahamiana na kutengeneza mazingira rafiki kwa pamoja na kupata matokeo chanya.

WTF imewapa ruzuku mashirika zaidi ya 200 yaliyo kwenye hali ya chini na pia mashirika yaliyo kwenye ngazi ya kitaifa tangu shirika hili lianze kufanya kazi mwaka 2011. Miaka mitano iliyopita, WTF ilifadhili programu ambazo zinahusika na mambo ya haki kwenye eneo la kukuza haki za kiuchumi kwa wanawake na wasichana, haki za uongozi na kuunga mkono harakati za elimu ya wasichana.

Kwenye mpango wa kusaidia harakati kwenye ngazi za chini kabisa, WFT imetenga asilimia 60 ya ruzuku zake. Hii inaenda sambamba na kutoa ushauri kuhakikisha washiriki wa ngazi za chini wanashiriki kwenye kampeni za kitaifa.

Yafuatayo ni mafaniko chanya yaliyowezeshwa na mfuko huu na kuleta mchango mkubwa:

Muungano juu ya haki za kikatiba za wanawake, uchaguzi na uongozi ambao una idadi kubwa ya mashirika ya haki za wanawake kama 80, mitandao, na vikundi vyenye utaalam mwingi katika utengenezaji wa sera na utetezi, mabadiliko ya sheria, kuandaa msingi, na uongozi wa wanawake wadogo.

Kampeni ya Kupambana rushwa ya ngono ni ajenda muhimu ya harakati za ukombozi wa wanawake na imeonyesha mashirika yaliyopokea ruzuku yanayoshughulika na jitihada zao zimetambuliwa kwa kiwango cha kitaifa na kushirikiana na watendaji wa serikali TAKUKURU

WFT inatoa msaada wa kitaalamu kupitia TAKUKURU ambao waliibua tatizo la rushwa ya ngono iliyo kwenye vyuo vikuu viwili. Vyuo hivyo ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Dodoma.
Washiriki wengine wa WFT waitwao WAJIKI walianzisha kampeni ya mlango kwa mlango miaka sita iliyopita kwa lengo la kupambana na rushwa ya ngono. WAJIKI walitumia madereva na wasaidizi wa madereva wa vyombo vya umma kama daladala, pikipiki na kuwatumia katika kukamilisha kampeni hiyo.
Kampeni hiyo ilitumia nyimbo, vipeperushi, fulana zenye jumbe mbalimbali za kupambana na rushwa ya ngono.
Mwaka 2020 kampeni ilifikai watu 45 na asilimia 72 ni wanaume. Kumekua na mabadiliko ya tabia na mtazamo kutoka kwa wanaume waliokua wakitaka rushwa ya ngono kutoka kwa wanafuzni wa kike na wasichana wadogo wasio na uwezo wa kulipa nauli baada ya kupata huduma ya kusafiri.

WTF imetengeneza jukwaa ambalo wanawake wanapeana uzoefu wa kianaharakati na ujuzi mbalimbali kupitia jukwaa la ‘Her story’. ‘Her story’ ina zaidi ya wanachama 35 ambao ni binafsi na taasis pia. Jukwaa hili linalenga kwenye kuzalisha, kutunza na kukusanya hadithi au habari zenye mlengo wa kianaharakati na kukuza ajenda ya kimaendeleo.

Groups

Members

Most Liked

Comments

    Featured