Upendo Chitinka

Utanzu: Michoro Picha (Comic) na Ushairi
Upendo ndio jina langu. Sanaa ndio fani yangu. Ushairi na michoro ya picha ndio zana zangu katika mapambano dhidi ya ukatili na unyanyasaji wa mtoto wa kike. Wito na dhamira yangu ni kusimamia haki na usawa. Upendo ndio ujumbe wangu. Upendo ndio jina langu.
NDOTO ZA BINTI
Shauku na matamanio yake ni kupiga makasia kwenye bahari ya maarifa, bahari isiyo na mwisho. Mawimbi makali yanamuandama na punde si punde anatandikwa na wimbi kubwa la kuolewa, angali bado mdogo na yuko mwanzo kabisa mwa safari yake baharini. Akiwa amekata tamaa, taarifa za mkasa wake zinaenea. ‘Si sawa! Si haki!’ manung’uniko kede yanasikika. Watu kadhaa wanajitolea kudai haki, wakiongozwa na mama yake.

InstagramEmailInstagram
Mary Rusimbi

Mary Rusimbi ni mwanamke Mtanzania ambaye ni mwanaharakati, mtafiti na mshauri wa masuala ya jinsia na maendeleo.
Kama mwanaharakati mwanamke amefanikiwa kuwa sehemu na mwanzilishi mshiriki wa Tanzania Gender Networking Program (TGNP) Ni mwanzilishi wa Women Fund Tanzania Pia ni mwanachama wa Foundation for Civil Society ambayo ni jumuiya inayojitegemea isiyo ya faida inayoziwezesha jumuiya nyingine kuwasaidia wananchi katika mchakato wa maendeleo na utawala bora
Mary Rusimbi ni mfeminia anayeendelea kuwashika wafeminia wachanga mkono

Lucy Lameck

Mwanaharakati mtanzania ambaye
1. Alipinga ukoloni wa Uingereza
2. Alipinga ubaguzi na alikuwa mtetezi mkubwa wa wanawake enzi za ukoloni.

Ushujaa wake ulipelekea wajerumani kubadili jina la barabara ya Wissmann na kuuita Lucy Lameck

Anaingia kwenye historia ya siasa za Tanganyika na baadae Tanzania ambapo ameshika nyadhifa za uwaziri
1. Waziri mdogo wa shirika la maendeleo ya jamii (1962-1967)
2. Naibu waziri wa afya (1967-1972)

Susan Geiger

Susan Geiger ni mwandishi ambaye historia ya wanawake nchini hasa wakati wa Uhuru na harakati zao.
Kitabu chake cha WANAWAKE WA TANU kimejaa taarifa muhimu za wanawake wanamapinduzi.

Sofia Kawawa

Mama Sofia Kawawa anafahamika sana kama mwananapinduzi na kiongozi wa umoja wa wanawake lakini mchango wake katika kuwezesha mabadiliko muhimu ya kisera kulinda wanawake na watoto ni mkubwa.

Getrude Mongella

Getrude Mongella kwa nafasi kubwa anafahamika kama kiongozi aliyeshika nyadhifa mbalimbali lakini hasa kwa mchango wake katika mkutano wa Beijing.

Litti Kidanka

Litti Kidanka ni mwanamke shujaa aliyewaongoza Wanyaturu katika mapambano dhidi ya utawala wa wakoloni wa kijerumani kati ya mwaka 1903 -1908. Alifanikiwa kuwasambaratisha askari Kwa kutumia nyuki na Mapambano hayo yalidumu Kwa miaka mitano.

Leila Sheikh

Leila Sheikh ni mwandishi wa habari wa Tanzania, mwanaharakati wa haki za wanawake na mhariri wa majarida. Alikuwa mwanachama mwanzilishi wa Chama cha Wanawake cha vyombo vya habari Tanzania (TAMWA) na kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA mnamo 1996 na pia mhariri wa jarida la TAMWA, Sauti ya Siti (Sauti ya Wanawake)
Alikuwa mhariri wa jarida la kwanza la haki za wanawake nchini Tanzania akiwa na umri wa aliona shida ya unyanyasaji wa kijinsia. Wanawake na watoto wakidhulumiwa na hakuna mtu yeyote aliyehangaika kwa hilo.Aliratibu timu, ambazo zilishawishi Sheria ya Makosa ya Kujamiiana (SOSPA).